PePhiLePan Group Limited

PePhiLePan Group Limited

Makala Zangu

MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI WALIOFANIKIWA KUPITIA KAZI ZA AJABU

1. JEFF BEZOS

Huyu ni mmiliki wa kampuni kubwa duniani ya Amazon ambaye kwa sasa ndio tajiri namba mbili duniani. Lakini Bezos kufika kuwa bilionea namba mbili duniani safari yake imetokea mbali. Kazi yake ya kwanza alikuwa mpishi tu, akiandaa vyakula kama baga katika kampuni ya McDonald. Alikuwa na umri wa miaka 16 tu wakati akifanya kazi hiyo na kulipwa dola $2.69, kwa lisaa limoja.

Mbali na Amazon pia anamiliki The Washington Post aliyoinunua mwaka 2017. Mwezi February 2021, Amazon ilitangaza kwamba Bezos atajiuzuli kama mtendaji mkuu wa kampuni hiyo kuanzia robo ya tatu ya mwaka huu.

Disemba 2013, Bezos alishika vichwa vya habari kwa kuanzisha majaribio aliyoyaita "Amazon Prime Air," ambayo ni utumiaji wa ndege zisizokuwa na rubani kupeleka huduma kwa wateja wake. Ndege hizo zinaweza kubeba vifurushi vyenye uzito wa mpaka kilo 2.5 na zinaweza kufika umbali wa mpaka maili 10 kutoka ofisi za usambazaji za Amazon.

2. ELON MUSK

Amekulia Amerika Kusini baadae akahamia Canada akiwa na umri wa miaka 17 na kuanzia kazi ya kawaida kabisa kama Mhandisi wa program za Kompyuta. Ilikuwa mwaka 1983 na alikuwa akiuza michezo ya kompyuta na kulipwa dola $500 kwa mwezi. Mwezi Januari 2021, Musk aliripotiwa kumpiku Jeff Bezos kama mtu tajiri zaidi duniani. Inasubiriwa ripoti ya mwaka 2021 kuona matajiri hao wako kwenye nafasi zipi.

Lakini sasa ni tajiri namba tatu duniani akiajiri maelfu ya watu kupitia makampuni zake za Tesla na SpaceX zinazotengeneza roketi, magari ya umeme, umeme wa jua na mabetri akitajwa kuwa na utajiri dola za kimarekani $168.2

Utajiri wake ulianza kukuwa kwa kasi akiwa na miaka kati ya 25 na 30, akianza kwa kuiuza kampuni yake ya mwanzo mwanzo tu ya Zip2 kwenda kuwa sehemu ya Compaq Computers. Wazazi wake walitengana akiwa na miaka 10 na hapo akanza kupenda masuala ya kompyuta.

Alijifunza mwenzewe namna ya kutengeneza program za kompyuta, na akiwa na umri wa miaka 12 tu akauza program yake ya kwanza, ilikuwa ya mchezo ya kompyuta(game) iliyoitwa Blastar, safari ya utajiri ikaanzia hapo, alikuwa akitengeza na kuuza kwa bei chee kidogokidogo baadae ujuzi wake ukampa fedha na kuwa mmiliki wa kampuni kubwa duniani ya masualoa ya teknolojia.

3. BILL GATES

Bill gates ni bilionea namba nne duniani anayefahamika sana na mmiliki wa kampuni ya Microsoft. Amekuwa na mchango mkubwa katika bara la Afrika kupitia taasisi yake na mkewe ya Bill & Melinda Gates Foundation ambayo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya kijamii.

Ameongoza pia kwenye zoezi la kusaidia chanjo ya polio kwa watoto barani Afrika. Lakini hakuanza kama bilionea, alianza kama mfanyakazi wa kawaida tu kwenye kampuni iliyokuwa ndogo ya TRW, alikuwa mtengeza program za kompyuta wa kampuni hiyo, lakini sasa ni bilionea namba 4 duniani akiwa na utajiri unaofikia dola bilioni $129.2 kwa mujibu wa Forbes.

Bill gates alikacha shule akiwa mdogo tu akiwa na rafiki ya wa utotoni Paul Allen na kuamua kuanzisha Microsoft. hakuwa anaeleweka na familia yake, lakini aliamini katika fikra zake na kwa kuanza kidogokidogo akajikuta anakuwa na kutengeneza utajiri wa kutosha.

4.WARREN BUFFET

Warren Buffet, mfanyabiashara na bilionea mkubwa Marekani ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Forbes anashika nafasi ya 9 kwa watu wenye utajiri mkubwa dunaini. Alianza kazi ya kusambaza magezeti tu mtaani, majumbani na maofisini akifanya kazi hiyo ya kusambaza magazeti ya The Washington Post na kulipwa kama dola $175 kwa mwezi.

Lakini sasa ni bilionea wa kutupwa akiwa mkurugenzi mtendaji wa wa makampuni ya Berkshire Hathaway nchini Marekani ambayo kwa ujumla yameajiri watu zaidi ya 360,000 na kwa mujibu wa taarifa rasmi za mwaka jana ilikuwa na utajiri wa dola bilioni 42.5.

Aiwa na miaka 11 alianza kuwekeza kwenye kampuni ya Cities Service Preferred akianza kwa kununua hisa tatu tu ambapo hisa moja iliuzwa kwa $38. Akauza hisa hizo kwa faida kiduchu kwa kuuza hisa moja kwa $40, baada ya thamani ya hisa za kampuni hiyo kushuka mpaka $27, baadae akajuta baada ya thamani ya hisa kupanda mpaka $200. Anasema majuto haya ndiyo yaliyomsukuma kufikiria zaidi uwekezaji na kuwa mmiliki wa kampuni kubwa usoni. Kufika huko ilipaswa awe na mtaji wa kuanzia, na kazi yake ya kusambaza magazeti ilikua moja ya njia ya kumfikisha alipofika sasa.

5. SAID SALIM BACKHRESSA

Ingawa si bilionea katika orodha tajika ya Forbes, lakini historia yake inamleta kwenye kundi la watu matajiri walioanza kufanya kazi za kawaida kabisa mpaka kuwa matajiri wakubwa Afrika. Ni milionea tajika Afrika akizaliwa visiwani Zanzibar, Tanzania.

Kama ilivyo kwa watoto wengi wa Tanzania na vijana wengi wa nchi hiyo, hupitia kufanya kazi nyingi za kawaida kutokana na uchumi uliopo na mazingira ya nchi hiyo. Bakhresa alianza kuuza mabaki ya mazao ya baharini tu yanayopatikana kwa wingi hata sasa kwenye fukwe za bahari katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Mombasa.

Bakhresa hakulala na kuamka tajiri bali alianzia mbali kuusaka utajiri wake. Alianza kwa kushona viatu, akauza urojo na viazi kabla ya kufungua mgawaha mdogo lakini leo makampuni yake kwenye sekta ya Usafirishaji, Vinywaji, vyombo vya habari, maji, vyakula, viwanda vya nguo, hoteli na vitu vingine ambayo yameajiri zaidi ya watu 2,000 na kuingiza mabilioni ya fedha.

Makampuni ya Said Salim Bakhresa & Co. (SSB), yananufaisha zaidi ya watu 6,000 kwa ajira rasmi na zisizo rasmi katika nchi za Afrika Mashariki. Bidhaa za makampuni yake zinapatikana karibu nchi sita za Afrika Mashariki. Mwaka 2008 alianzisha mpango wa kukabiliana na Malaria baada ya utafiti kuonyesha mfanyakazi wake mmoja kati ya watano hukumbwa na malaria kila mwezi.


MAMBO YA AJABU YALIYOGUNDULIWA SAYARI YA MARS.

Na. Peter P. Panduka

Sayari ya Mars imekuwa ikiwashangaza, kuwasisimua na kuwavutia binadamu kwa miaka mingi.

Maelfu ya miaka iliyopita, binadamu walikuwa wakishangaa na kujiuliza nini kinapatikana katika sayari hiyo inayopatikana umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka kwa dunia (maili milioni 34).

kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu sawa na ya chuma iliyoshika kutu, binadamu waliihusisha na moto au damu.

Jina Mars linatokana na mungu wa vita wa Warumi.

Kutokana na ufanisi wa kisayansi, binadamu kwa sasa amefanikiwa kufahamu mengi kuhusu sayari hii.

SAYARI HII INA MANDHARI YA KUSHANGAZA: utayapata maeneo sawa na ya nyika duniani, maeneo ya jangwa kutokana na upepo mkali, mashimo makubwa yanayotokana na volkano, milima ya volkano na maeneo ya ukubwa sawa na taifa la Luxembourg yaliyojaa milima (machungu) ya mchanga.

Haya yote yamefunikwa na vumbi ya rangi moja.

Ni eneo ambalo huwa hakuna mvua kamwe. Hakuwezekani kuwa na mvua kwani maji, iwapo yangekuwepo, hufusha na kuwa mvuke mara moja.

Katika sayari ya Mars, wakati sawa na wa kutua kwa jua duniani, anga hujaa rangi ya buluu. Dunia huonekana tu kama nukta tu miongoni mwa nyota angani.

Ni mandhari ya kupendeza sana hasa kwa wanaopenda utalii - ikizingatiwa kwamba binadamu hajatalii sana sayari hiyo, kuna uhakika kwamba iwapo utafanikiwa kufika huko, kila utakapoenda utakuwa binadamu wa kwanza kufika huko.Utakuwa kama Wazungu waliokuwa wanatalii Afrika karne ya 19, ambapo walikuwa Wazungu wa kwanza kutazama milima, mito, nyika na misitu ya kupendeza barani. Lakini kumbuka kwamba hakuna oksijeni.

UTAFIKAJE HUKO?

Kwa karne nyingi, imekuwa ndoto tu lakini inakaribia kutimia. Iwapo mambo yote yatakwenda sawa, mjasiriamali mmiliki wa Space X Elon Musk anapanga kutuma kundi la kwanza la watalii kwenye sayari hiyo kufikia 2022.

Lakini gharama yake itakushangaza pengine. Tiketi ni $10bn! Lakini iwapo huwezi kupata pesa nyingi kiasi hiki, usife moyo. Kuna njia nyingine ya kiteknolojia ambayo taasisi ya safari za anga za juu ya Marekani Nasa inatafakari - kutumia miwani ya kisasa na roboti. Roboti ndiyo itakuwa Mars, wewe uwe  hapa duniani lakini itakuwa ikikupeperushia picha za uhalisia kutoka sayari hiyo.

VIVUTIO SAYARI YA MARS

Kivuti kikuu ni mlima wa Olympus Mons. Mlima huu una urefu wa maili 14 (kilomita 22), na ndio mlima wa volcano mrefu zaidi katika Mfumo wa Jua. Kwa kulinganisha tu, urefu wa mlima huu ni mara tatu urefu wa mlima mrefu zaidi duniani, Mlima Everest.

Sawa na ilivyo kwa milima mirefu ya volkano duniani, mlima huu kilele chake kimefunikwa na mawingu - lakini si ya maji, bali ni ya vumbi.

Haijabainika iwapo mlima huu bado hulipuka, lakini inakadiriwa kwamba wakati mmoja ulilipuka na kurusha matope na mawe makubwa ya moto angani.

Ukisafiri kusini magharibi kutoka kwa mlima huu, utapata Valles Marineris.

Hili ni bonde, linakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 4,000 ambao ni karibu na upana wa taifa la Marekani kutoka mashariki hadi magharibi.

Katika baadhi ya maeneo, bonde hili lina kina cha karibu kilomita saba (futi 23,000) - karibu mara nne kina cha bonde maarufu la Marekani ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Grand Canyon.

Milima mingi Mars ina mito midogo ambayo inadhaniwa kuwa inatokana na michirizi ya maji yenye chumvi

Kufikia sasa, haijabainika bonde kubwa kiasi hiki liliundwa.

Bonde hili la Valles Marineris lina mchanga wenye marangi mbalimbali ya kupendeza ambao umejipanga kwa safu mbalimbali. Inadhaniwa kwamba huenda mchanga huu ulitokana na mashapo au machenga ambayo yalijikusanya chini ya ziwa au mto wa barafu, au kutokana na kujikusanya kwa majivu ya volcano.

Kinyume na bonde la Grand Canyon Marekani, ambalo liliundwa na mmomonyoko uliochota mchanga na kuyachonga mawe, kuna uwezekano kwamba bonde hili la Mars lilitokana na kutengana kwa maeneo mawili makubwa ya 'ardhi' ya Mars. Kila upande wa bonde hilo unaweza kuingia kwa ule mwingine, kana kwamba mtu anajaza mchezo wa fumbo.

Wakati wa kutua kwa jua, anga huwa la rangi ya samawati

Ukafanikiwa kujipata kwenye bonde hili, na uwe unataka kuangalia kutua kwa jua, utashangaa kugundua kwamba anga lake halitakuwa ya rangi nyekundu - bali ya samawati. Hii inatokana na wepesi wa anga la sayari ya Mars, ambalo ni asilimia moja tu ya uzito wa anga la Dunia.

Anga la Dunia huwa rangi ya samawati mchana kutokana na miali ya jua kutawanywa na molekuli za hewa. Hili huwa halitendeki sana sayari ya Mars, hivyo mchana anga huwa la rangi ya manjano iliyokaribia hudhurungi. Lakini jua linapotua, ambapo miali yake huwa haina nguvu sana ndipo anga la Mars hugeuka na kuwa rangi ya buluu.

Sayari ya Mars pia ina jambo jingine la kushangaza. Katika maeneo mengi, chini ya vumbi lake jekundu, kuna mawe ya rangi ya samawati na kijani kutokana na madini kama vile chuma. Vumbi hilo linapobebwa na upepo au kutokana na kupita kwa sayari ndogo, huwa kunafichuliwa mandhari ya kupendeza ya mikolezo tofauti ya rangi ya samawati.

HALI YA HEWA

Kiwango cha joto cha kadiri katika sayari ya Mars ni nyuzi joto takriban -56C (-69F). Hii ni sawa na hali ya baridi maeneo ya ndani kabisa ya Antarctica, anasema mtaalamu wa biolojia na anga za juu katika Chuo Kikuu cha Washington, David Catling.

Ndipo uweze kufurahia, itakubidi kukaa karibu na ikweta ya Mars, ambapo huko kiwango cha joto kinaweza kufikia takriban 35C (95F), na hakuna upepo sana. Kutokana na wepesi wa anga lake, upepo mkali huko utahisi kana kwamba ni upepo tu Ingawa huwa kuna unyevu na ukungu usiku katika sayari hiyo, mchana hali ni kavu sana.

Kutokana na hali kwamba sayari hiyo inapatikana karibu mara moja unusu mbali na jua ukilinganisha na Dunia, hakuna haja ya kuvalia miwani ya kukinga dhidi ya mwanga wa jua.

Huko, kuwasha moto pia ni ngoma kwani hakuna mimea na anga lake asilimia 96 ni kaboni daoksaidi - kemikali inayotumiwa kwenye mitambo mingi ya kuzima moto.

Tofauti na Dunia, ambapo mawingu na anga hufanya kazi kama blanketi na kuzuia joto kuondoka usiku, sayari ya Mars hakuna mawingu na anga lake ni jepesi sana. Matokeo yake ni kwamba, sawa na inavyofanyika jangwani, usiku huwa kuna baridi kali sana. Baridi hii inaweza kufikia nyuzi -73C (-99F) usiku karibu na ikweta kwenye sayari hiyo.

KUNA VIUMBE HAI?

Viumbe wote walio hai duniani huwa wana maji ndani yake. Hivyo, wataalam wamekuwa wakiamini kwamba iwapo kuna viumbe Mars, lazima wawe kwenye maeneo yaliyo na maji.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walitafuta ishara za kuwepo maji Mars bila mafanikio.

Lakini mwaka 2011, walifanya ugunduzi huo. Waligundua michirizi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwa milima na mabonde ya Mars. Inadhaniwa kwamba huenda mito, yenye maji yenye chumvi labda huchipuza kutoka chini ya 'ardhi' kwenye hazina kubwa ya maji.

BINADAMU HUBADILIKA?

Kutokana na kiwango cha chini ya nguvu mvuto, uzani wa vitu huwa tofauti sayari ya Mars. Binadamu wa kilo 100 hivi, uzani wake Mars unaweza kuwa karibu na kilo 38 hivi.

Ukafanikiwa kutua kwenye Mars, utakuwa ukiitazama Dunia na kuiona kama tone au kituo angani. Dunia utaiona ikiwa sawa na tunavyoiona sayari ya Zuhura mapema asubuhi, au jioni angani.

Photo by
X