MAKALA KUNTU
MWANDISHI ALIETHAMINI UTUNZI KULIKO PESA
Makala hii inamuhusu Gwiji la uandishi wa novel "King James hardley Chase"
Nimemtunuku ufalme, kwa sababu anastahili hicho cheo kwenye tasnia ya utunzi, Uzuri hakuna anaesomea uandishi, Uandishi ni taaluma iliyo ndani ya Mioyo ya watu wachache waliotunukiwa, kiufupi tuseme uandishi ni kipaji tu!!, kinyume na hapo unaweza kwenda shule ukasoma mpaka ukawa Professor ila kutunga hadithi ya Fiction kwako kunaweza kukakupiga chenga🤪, Sio jambo la ajabu hata kidogo!!!!
Kama ilivyo kwa waandishi wengii duniani, Hupenda zaidi kunufaika na stori ambazo kiundani wao si watunzi, kuna waandishi mbalimbali mfano ushawahi kumsikia J.K.Rowling?
Jamaa mmoja alinufaika sana kwa kudai kuwa yeye ni JK Rowling, alipewa mpaka Tuzo za Dunia, kumbe Wala sio yeye, Ajabu kwelii!!!!
Mwisho wa siku mwandishi huyo alieficha uhusika wake akajitokeza baada ya miaka 5 ya kuficha uhusika wake, Dunia ikamfahamu Kama Jane K Rowling mwana mama alieandika mifululizo ya vitabu vya HARRY POTTER, Kisa cha yeye kuficha uhusika ni kwamba Kama angefahamika kuwa yeye ni mwandishi mwanamke hivyo asingeuza!!! Ama kweli watu Wana strategy zao bhana!!!
Wimbi la waandishi kununua hatimiliki za stori zisizo zao lilikuwa gumzo kwelikweli kwenye miaka ya 1960 kwasababu uandishi ni Pesa, Hasa ukiwa Mtunzi mahiri wewe umeshajifikia mawinguni kitambo sana.
Mafanikio ni kitu ambacho wengi huyatamani sana tena Hasa yale ya kiuchumi, Ila kwa James hardley Chase mambo yalikuwa ni tofauti... Sasa Fuatana nami👇👇
James Hardley Chase alizaliwa tarehe 24 December 1906, Jina lake la kuzaliwa ni Rene Lodge Brabazone Raymond, Jamaa alikuwa na jina refu, huku Tanzania namfaninisha Kama ditopile ila ni kwenye urefu wa majina peke yake na sio vitu vingine.
Alijulikana kwa majina Lukuki, yaani jamaa alikuwa anabadili majina kulingana na mazingira yake binafsi ( Alitumia majina Kama James L Docherty, Raymond Marshall, na Ambrose Grant) wakati mwingine aliyatumia majina haya Kama Mtunzi kwenye vitabu vyake mbalimbali ila watu waligundua kuwa ni yeye, Hivyo wakambatiza jina la JAMES HARDLEY CHASE (THE CHASE).
Mpaka kufikia miaka hio ya 1984 alishajizolea karibia Tuzo 90, na kumfanya kuwa mwandishi bora wa wakati wote. CHASE ni mtoto wa kwanza wa Colonel Brabazone Raymond, Baba yake alipenda sana mwanae asomee Sayansi, hivyo ilimbidi ampeleke kwenye shule za hadhi sana pale uingereza The King's school Rochester.
Ila alipofikisha umri wa miaka 18, Chase alitoroka Nyumbani, akaenda kufanya kazi za uuzaji wa vitabu katika maktaba kubwa ya vitabu jijini London, Alikuwa anapenda kusoma Vitabu na pia alipopata Fursa ya kukutana na wateja aliwashawishi kununua vitabu huku akiwasimulia mambo yaliyoandikwa katika vitabu hivyo.
Chase aliitambua roho ya uandishi aliokuwa nayo mapema sana, Kama nilivyodokeza uandishi ni kuyaona yasiyoonekana na kuvipa uhai kupitia maandishi, ama kweli Chase hakufanya mzaha katika hilo.
Baada ya Anguko la Uchumi wa Dunia ( THE GREAT DEPRESSION 1929-1939), Kundi la Chicago gangster lilipata umaarufu kutokana na kuhusishwa katika uporaji na ubakaji. Chase aliliona Kundi hilo Kama Fursa yake ya utunzi wa stori za FICTION ama Thriller.
Alichapisha kitabu chake cha kwanza mwaka 1939 kilichoitwa NO ORCHIDS FOR MISS BLANDISH ( Hakuna Bustani kwa mlimbwende BLANDISH).
Kipindi cha vita vya pili vya Dunia, The chase alijenga urafiki na Merrill Pannit (Muongozaji vipindi vya Televisheni) Aliempatia Chase kamusi yenye maneno ya kiingereza kile cha watu weusi. Chase hakuwahi kuishi marekani ila alikipenda kiingreza kile cha watu weusi kilivyokuwa kikitoka kwa mtindo wa kufoka na kejeli nyingi yaani "SLANGS".
CHASE alidhamiria kukiingiza kiingreza hicho katika uandishi, jambo ambalo lilimpa umaarufu mkubwa sana mpaka hii leo, Mwaka 1940 aliandika THE VILLAIN AND THE VIRGIN ( Mwovu na Bikira), kitabu hichi kikampaisha sana Chase na akafululiza kutoa vitabu vingi Kama The dead stay Dumb ( wafu hukaa bubu), Get a Load of this ( Pata mzigo wa hii), The flesh of the orchard ( Nyama ya Bustani), Lay her among the Lilies ( Muweke Kati ya Mayungiyungi) na I would rather stay poor ( Bora nibakie masikini).
Hakuthamini sana Pesa, aliamini bila utunzi kwake hakuna Maisha, hakuwahi kusema kuwa kitabu hichi sijauza Kama kile, ila alisikika akisema watu wasome wajitengenezee taswira itakayowaongezea ujuzi na ufahamu. What a writer!!!
Aliwapenda watu sana na aliipenda tasnia ya uandishi, ila kumbuka ni msomi wa ngazi ya kusoma na kuandika na kuhesabu tu 🤪🤪, Alipenda kuandika stori zenye visa vigumu kueleweka, Lengo lilikuwa ni kufungua Bongo za vizazi vyote vitakavyosoma kazi zake.
Mpaka kufariki kwake mwaka 1985, aliuza vitabu vyake vingi katika nchi za Ufaransa, uingereza na Marekani, Sifa yake kubwa ni kuuthamini Utunzi, alikula kupitia utunzi mpaka mauti inamkuta. Ndio maana tukasema ni mwandishi aliethamini utunzi kuliko Pesa 🤪🤪,
Mwaka mmoja kabla ya kifo chake aliiachia Dunia utunzi ambao hautakuja kufutika kamwe, ni kupitia kitabu chake alichokiita HIT THEM WHERE IT HURTS ( Wagonge mahali palipoumia) kitafute kitabu hicho na ukisome!! Sasa shauri yako!!!
Vitabu vyake 30 vilitumika kutengenezea Filamu 30 huko Ufaransa. Mpaka mauti inamfika, James hardley Chase ameandika vitabu 50 vya Fiction.
TUKUTANE KWENYE MAKALA NYINGINE, HAPA SINA LA ZIADA, NASHUKURU 🙏🙏
HISTORIA ILIYOJIFICHA KUHUSU KUANZISHWA KWA TAWALA YA ROMA (ROMAN EMPIRE)
SIKU HII KATIKA HISTORIA
APRILI 21
753 B.K.
Aprili 21
Roma ilianzishwa
Roma kwa Sasa inajulikana Kama Taifa la Itali au ukipenda unaweza kuwaita Warumi, Taifa la watu wabishi na wakorofi kwelikweli na wenye ukomavo wasiopenda kushindwa iwe katika vita, michezo na mambo mengine ya kisiasa.
Taifa mpaka kufikia hatua ya kuitwa taifa lazima liwe na mipaka, Utawala na miundombinu bora ya kufanya mahitaji ya wakazi wake kupatikana.
Kuna msemo unasema huwezi jenga Roma kwa siku Moja, msemo huu unaambatana na Historia ya kuanzishwa kwa taifa la roma ambayo ni ya ajabu sana pia na yenye kusisimua, Taifa lililoitawala Dunia na kuifanya isiweze kujitolea maamuzi yeyote katika Rasilimali.
Ikumbukwe warumi ndio waanzilishi wa miundombinu Kama Barabara, Mahakama na Mashule wakishirikiana na wagiriki, walijizatiti katika kuwekeza kwenye majeshi yao yenye nguvu kubwa ambayo yalipitia chini ya uongozi mahiri wa majemedari mbalimbali akiwemo kamanda Titto, kamanda Vasilius na wengineo wengi walioitikisa Dunia.
Tuanze Historia ya kale sana inayoihusu Roman Empire, Sasa twende kazii..
Kulingana na jadi, mnamo Aprili 21, 753 KK, Romulus na pacha wake, Remus Ndio waanzilishi wa Roma. Hii ilikuwa ni katika makuzi yao wakipitia kipindi cha ajabu cha kunyonya maziwa ya mbwa mwitu kama watoto yatima, mara baada ya kutelekezwa.
Kwa kweli, Historia ya Romulus na Remus ilianzia wakati fulani katika karne ya nne KK, na tarehe halisi ya kuanzishwa kwa Roma iliwekwa na msomi wa Kirumi Marcus Terentius Varro katika karne ya kwanza B.K.
Kulingana na historia, Romulus na Remus walikuwa wana wa Rhea Silvia, binti wa Mfalme Numitor wa Alba Longa. Alba Longa ulikuwa mji ulio katika Milima ya Alban kusini mashariki mwa Roma.
Kabla ya kuzaliwa kwa mapacha, Mfalme Numitor aliondolewa madarakani na kaka yake mdogo Amulius, ambaye alimlazimisha Rhea kuwa bikira wa kupendeza ili asizae kwasababu aliamini kupitia uzao wa Rhea wangezaliwa wapinzani kwa jina lake.
Walakini, Rhea alipachikwa mimba na mungu wa vita Mars (Moja ya Miungu ya Kirumi ya kivita) na akamzaa Romulus na Remus.
Amulius aliamuru watoto wachanga kuzama ndani ya Tiber, lakini walinusurika na kuibukia pwani chini ya kilima cha Palatine, ambapo walinyonyeshwa na mbwa-mwitu.
Hii ilikuwa ni baada ya mbwa mwitu kuwaona watoto wadogo wachanga ambao hawakuwa na tumaini lolote la maisha, Mbwa mwitu huyo aliwasogelea na ghafla mapacha hawa walilia kulalamika kuwa wanahitaji maziwa (ishara katika lugha ya watoto ) Mbwa mwitu huyu hakuwa na hiana kwa kuwa alitoka kuzaa punde hivyo ikambidi awanyonyeshe Hawa watoto wa Binadamu ( Hili jambo ni halisi). hadi walipopatikana na mchungaji Faustulus. mfugaji aliependa kuchunga mifugo yake mwenyewe.
Walilelewa na Mfugaji huyu Faustulus na mkewe, mapacha hao baadaye wakawa viongozi wa bendi ya vijana mashujaa wachungaji.
Baada ya kujifunza kuhusu utambulisho wao halisi, waligundua kuwa wao ni Wana ufalme hivyo walijiimarisha kijeshi na kumshambulia Mfalme Amulius muovu, na kumrudisha babu yao kwenye kiti cha enzi.
Mapacha Hawa waliamua kujenga mji kwenye sehemu ambayo walikuwa wameokolewa kama watoto wachanga.
Baada ya kukamilisha mji walioujenga Kama kumbukizi ya Historia yao, walihusika katika ugomvi mdogo, ambao ulipelekea Remus kuuawa na kaka yake.
Romulus akawa mtawala wa makazi, ambayo iliitwa "Roma" baada yake. Hivyo neno Roma lilitoka kwenye jina la Romulus, kijana aliemuua ndugu yake waliotaabika pamoja na kufanya mambo mengi pamoja, ila kutokana na uchu wa madaraka akafanya machafuko hayo yote.
Tamaa ya Romulus ya madaraka, hata baada ya kufa kwake ikaendelea kurithiwa na vizazi mpaka vizazi. Ama kweli huwezi jenga Roma kwa siku Moja, hivyo ni kutokana na usaliti na udhandiki ulioshamri enzi hizo, Figisu zilikuwa nyingi sana, kiasi cha kwamba jambo la kubadilisha mfumo wa utawala lilichukua karne na karne za miaka.
Naam Asanteni, Hiyo ndo historia ya kuanzishwa kwa urumi yaani Roma, lililotoholewa kutoka kwa kijana Romulus. Tukutane katika makala ijayo.
IFAHAMU HISTORIA YA CHUO CHA SOKOINE CHA KILIMO ( SUA )
Historia ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine inaanza mwana 1965, ambapo kilianzishwa kikiwa Chuo cha Kilimo kilichokuwa kinatoa mafunzo ya kilimo kwa ngazi ya diploma.
Kufuatia kuvunjika kwa kilichokuwa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na kuanzishwa rasmi kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1970, chuo hiki kilibadilishwa na kuwa Kitivo cha kilimo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuanza kutoa Shahada ya Sayansi katika Kilimo.
Mwaka 1974, Kitengo cha Misitu kilianzishwa na hivyo taasisi nzima ikanbadilishwa jina na kuitwa Kitivo cha Kilimo na Misitu. Kufuatia kuanzishwa kwa Shahada ya Sayansi za Tiba ya Mifugo mwaka 1976 pamoja na kuanzishwa kwa kitengo cha Utabibu wa Migugo, jina la taasisi likabadilishwa tena na kuwa Kitivo cha Kilimo, Misitu na Sayansi za Tiba ya Mifugo.
Julai 1 1984, kitivo kilibadilishwa kwa Sheria ya Bunge Na.6 ya mwaka 1984 na kuwa Chuo Kikuu Kamili na kupewa jina la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kikiwa na vitivo vitatu; Kilimo, Misitu na SayansiTiba za Mifugo.
Hadi sasa, chuo kina vitivo vinne; Kitivo cha Kilimo, Kitivo cha Misitu na Uhifadhi, Kitivo cha Sayansitiba za Mifugo na Kitivo cha Sayansi.
Kwa sasa chuo kina kampasi nne; Kampasi Kuu iliyopo Manispaa ya Morogoro, Kampasi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu, Morogoro, Msitu wa Mafunzo Omolonyi, uliopo Arusha na Pori la Akiba la Mazumbai lililopo Manispaa ya Tanga.
Kwa sasa chuo kinatoa kozi 30 za shahada ya kwanza na kozi 45 za uzamivu.
Kampasi kuu ipo Manispaa ya Morogoro, mwendo mfupi kutoka Stendi Kuu ya Msamvu.